Social Icons

Monday, 31 October 2011

YANAYOJILI WATANI WA JADI WANAPOKUTANA

MASHABIKI WA YANGA WAKIWA NA BENDERA YENYE PICHA YA MTANI WAO
Mahabiki wa timu ya Yanga, wakiingia kwa mbwembwe uwanja wa Taifa huku wakiwa na Bendera yenye picha ya mtani wao wa Jadi ambapo furaha hii ilidumu hadi mwisho wa mchezo huo. MATANI YA WATANI WA JADI, MTANI NANI ALIMFUNIKA MWENZAKE????
MASHABIKI WA SIMBA WAKIWA NA JENEZA LA PAPIC Mashabiki wa timu ya Simba wakiingia kwa mbwembwe uwanja wa Taifa huku wakiwa wamebeba Jeneza lenye jina la Kocha wa Yanga Papic, lakini mwisho wa mchezo huo jeneza hili halikuonekana lilipopitia. MATANI YA WATANI WA JADI MTANI NANI ALIMFUNIKA MWENZAKE???
Picha kwa Hisani ya Sufiani Mafoto blog

Is 160 enough? One Indian man's family





Mizoram, India (CNN) -- The world's population hits 7 billion this week, but Ziona, the patriarch of what may be the biggest family in the world, is not bothered.
"I don't care about overpopulation in India ... I believe God has chosen us to be like this (have big families). Those who are born into this family don't want to leave this tradition so we just keep growing and growing," he says with a smile.
Ziona, who only goes by his first name, has 39 wives, 86 children and 35 grandchildren.
Ziona's father, Chana, founded the Christian sect in Baktwang village that promotes polygamy as God's will. "I never wanted to get married but that's the path God has chosen for me," he says. "It's not my wish to keep marrying again and again."
All 160 family members live in a four-storey mansion perched on top of a remote village in the northeastern Indian state of Mizoram.
The state, neighboring Myanmar and Bangladesh, has one million residents, one of the lowest population densities in this country of 1.2 billion. Despite its natural beauty, special permits are required to enter the state, making tourism virtually non-existent.


©Fredy Njeje

22 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA CHAD.


KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.
Mchezaji aliyeitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Mwandini Ally wa Azam huku pia akimjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas Ulimwengu.
Kikosi kamili ni makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba).
Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba).
Washambuliaji katika kikosi hicho ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), Hussein Javu (Mtibwa Sugar) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Timu itaingia kambini Novemba 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 9 mwaka huu kwenda N’Djamena kwa ajili ya mechi hiyo. Stars na Chad zitarudiana Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Tukio La Safari ya Miss Vodacom Tanzania 2011 katika kuelekia Fainali za mrembo wa Dunia

 Hapa Miss Vodacom Tanzania 2011 akiwa katika Vazi la Ufukweni na Wenzake katika maonesho ya Mavazi hayo
Hapa Miss Vodacom Tanzania 2011 akiwa katika pozi na Vazi lake la Ufukweni 

  Miss Vodacom Tanzania 2011 wa Kumi kutoka kulia akiwa na wenzake katika Dina la nguvu Huko Scottish maeneo ya Scottish Hydro 
 Miss Vodacom Tanzania wa Sita kutoka kulia akiwa bize anachukua Video wakati wakipata burudani ya nguvu huko Scottish maeneo ya Crieff Hydro
Miss Vodacom Tanzania 2011 akiwa na wenzake huko Scottish maeneo ya Crieff Hydro
Miss Vodacom Tanzia  aliye vaa Nguo za Njano katika maandalizi ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania

Picha hii na Ya juu take Miss Vodacom Tanzania 2011 wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia
Miss Vodacom Tanzania wa Tatu  kutoka kulia akifurahia kwa Shangwe wakati wa  Highland Games kuelekea kinyang'anyiro cha Mrembo wa dunia
Miss Vodacom Tanzania 2011 wa kwanza kushoto aliye simama akiwa katika picha ya pamoja na wenzake 
Miss Vodacom Tanzania 2011 wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi  na wenzake .. katika safari  ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia.


Picha zote hizi zimetoka katika page maalum ya Miss World lakini nimejitahidi kusaka picha zote ambazo Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel .. Endelea kufuatilia tukio hili nitawaletea kadili navyo pata tukio zima.
©Fredy Njeje

Miyeyusho amchakaza Matumla usiku wa leo

Bingwa Mpya wa UBO katika uzito wa Bantum,Francis Miyeyusho akifurahia ubingwa wake huo wakati akivishwa mkanda wake na Mlezi wa Mchezo wa Ngumi hapa nchini,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Afande Suleiman Kova huku Diwani wa Kinondoni,Mh. Abbas Tarimba akiangalia.Francis Miyeyusho kanyakuwa ubingwa huo baada ya kumchakaza vibaya Bingwa wa Zamani UBO,Mbwana Matumla katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall.
Bondia Francis Miyeyusho ampatia konde kali sana mpinzani wake,Mbwana Matumla wakati wa mchezo wao uliomalizika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall.Francis Miyeyusho kanyakua ubingwa katika mchezo huo kwa kushinda Mbwana Matumla kwa point.

Sunday, 30 October 2011

MOTO WA REDD’S UNI – FASHION BASH 2011 VYUO VYA DAR ES SALAAM WASHINDI WAPATIKANA



Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi akimkabidhi zawadi msindi wa kwanza wa Mitindo katika Tamasha la Redd’s Uni-Fashion Bash,Marvin Peter.
Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original,Victoria Kimaro akikabidhi zawadi ya mshindi wa Kwanza wa Ubunifu,Jackson gumbala (Udsm).

Kinywaji cha Redd’s Original kinachotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kesho kitafanya tamasha lake la kwanza kwa wabunifu na wanamitindo wa vyuo vya Dar es Salaam. Tamasha hili lijulikanalo kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” lilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi October likiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya wabunifu na wanamitindo walioko katika vyuo vya elimu ya juu.

Tamasha la fainali za jana zilikuwa na mvuto wa kipekee na lenye mvuto mkubwa, Ambapo washiriki walifanikiwa kuonyesha ubunifu mkubwa na umahiri wa hali ya juu tofauti na matarajio ya walio. Fainali za tamasha la Redd’s Uni – Fashion Bash kwa vyuo wa Dar es Salaam lilifanyika katika ukumbi wa FPA Uliopo chuo kikuu cha Dar Es Salaa karibu na Benk ya CRDB (Udsm) hapa Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni na kumalizika usiku wa manane.

Tamasha limeonekana kuwa na maandalizi makubwa kuanzia kwa majaji ambapo waliweza kutoa vigezo mbalimbali na namna wabunifu na wanamitindo wanapaswa kuwa.

Washindi katika tamasha la jana

a)Mitindo

1.marvin peter (Ustawi wa jamii)
2.Benson Macha(Cbe)
3.Asha Mohamed (TIU)
4.Yusuph Fanuel (Cbe)
5.Aloycia Innocent (Udsm)

Ubunifu ni

1.Jackson gumbala (Udsm)
2.Esther Amos(Cbe)
3.Mirium kairus(IFM)
4.Shabani (Udsm)

Ambapo waliweza kukabidhiwa zawadi zao pale pale ukumbini toka kwa wadhamini wa shindano hilo kampuni ya bia nchini Tbl kupitia kinywaji chake cha Redds Original.

Aidha shindano hilo lilikuwa na burudani mbalimbali zilizoandaliwa na Redd’s Original ambapo wasanii Roma Mkatoliki na John Makini walitoa burudani ya kutosha, pia

Akizitaja zawadi za washindi Bi Kimaro alisema; Redd’s Original pia itatoa zawadi kwa washindi kama ifuatavyo;
WABUNIFU
MSHINDI WA KWANZA 700,000
MSHINDI WA PILI 500,000
MSHINDI WA TATU 300,000
MSHINDI WA NNE NA WA TANO 100,000 KILA MMOJA

WANAMITINDO
MSHINDI WA KWANZA 500,000
MSHINDI WA PILI 400,000
MSHINDI WA TATU 300,000
MSHINDI WA NNE NA WA TANO 100,000 KILA MMOJA


Wasiriki walioingia fainali kwa mkoa wa Dar Es Salaam ni. 1.Aloycia Innocent (USSM)2.Rosemary Osward (CBE).3.Magreth Mhoza (MNMA.4.)Upendo Kuboja(CBE)

5.Kudra Lupatu (CBE)6.Emmanuel Elly (CBE).7.Lameck Stephen (IFM)

8.Benson Macha(CBE) 9.Saadat Juma Saadat (IFM)10.Conrad Gumbo(IFM)11.Issack Ibrahim(UDSM)12.Amos Kalinga(UDSM)13Asha Mohamed(KIU)14.Rose Hubert

(KIU)15Gerald Kalinga(UDSM)16.Hussein Kasimu(UDSM)17.Happyness Mushi(CBE)

18.Yalita Malanduzi(UDSM)19.Brian Abdul(CBE)20.Rosa Damazo(IFM) na majaji wa fainali hizi watakuwa 1.Taji Liundi 2.Farouk Abdala,3.Hamissa Hassan 4.Castantine Magavile.

Tamasha linalofuata linafanyika jumamosi ya November05 mjini Moshi mkoani kilimanjaro ambapo wanafunzi waliopo kwenye vyuo vya mkoa wa kilimanjaro wananafasi ya kuonyesha uwezo wao kwenye Tamasha hilo la aina yake hapa nchini Tanzania ambapo burudani zitaongozwa na wasanii Roma mkatoliki,Joh Makini na wengineo wengi.


©Fredy Njeje

I Just Chill Out and Perform Live @ Karaoke.. It was so Nice

 Before Entering to the Karaoke ... you need to prepare well ya Vocal
 I was Waiting a Drink ... 
 Microphone Test... 
After Singing some song i Get time for resting for a while 
I was so High During this song....

After That i Enjoy the Real Chinese Food which was so Delicious 

©Fredy Njeje

Jay-Z, Kanye West's Throne Tour Has Thrilling Liftoff

 Jay-Z and Kanye west























TLANTA, Georgia — Not even a stormy night could stop the regal reign of the Throne. On Friday, Jay-Z and Kanye West opened up their Watch the Throne Tour in Atlanta. While the WTT album has been noted for its opulent displays of wealth, Hov and Yeezy's show will be marked by the duo's overabundance of hit records.

The doors to the Philips Arena opened at 7:30 p.m. ET and, with no scheduled show opener, the house DJ played old slow jams like the Isley Brothers' "Between the Sheets," Little Beaver's "Get Into the Party Life" and Hank Crawford's "Wildflower" — all songs that have been sampled by Kanye and Jay at one time or another. Still, the subtle measure wasn't nearly enough to keep fans satisfied. By 9 p.m. ET, the crunked-up crowd was restless and salivating for the night's stars.
With the house lights low and fans pumped, the multilayered instrumental from "H.A.M." came blaring through the sound system. The initial WTTtrack has been criticized by some as too over-the-top and too much unlike anything in Jay and 'Ye's respective catalogs, but the helter-skelter mix of crashing symbals, bleeps, beeps and bombastic bass was clearly built specifically for sports stadiums and grand auditoriums.
The build was perfect, even if the execution wasn't. Kanye commandeered a rising platform at the front of the stage, while Jay simultaneously occupied a similar lift that was situated on the floor in the middle of the crowd. Within moments, the duo were elevated in unison towering above the audience, volleying verses from one side of the arena to the other. Jay stumbled vocally, though: His ear piece short-circuited and failed to properly feed him the music and his timing was clearly affected. For a time, Hov's raps were badly off beat.


Sherehe za kutimiza miaka Mitano ya 8020 Fashion Blog zafana leo

Shamim Zeze akimkaribisha mgeni rasmi ,Mh Angellah Kairuki kuzindua nembo ya mavazi (B2A) kama ionekavyo pichani,mbele ya wagine waalikwa mbalimbali walifika kwenye hafla hiyo ambapo kinywaji cha Baileys kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd,ilkuwa ni sehemu ya wadhamini.
Pichani Shamim Mwasha akikata keki ikiashiria kutimiaza miaka 5 ya blog yake ya 8020 anayoimiliki,kati ni mgeni rasmi Mh.Angellah Kairuki pamoja na Mwanyekiti wa Tanzania Mitindo House,Khadija Mwanamboka wakilishuhudia tukio hilo adhimu.
Mke wa ankal Michuzi akimlisha keki mgeni rasmi,Mh Angellah Kairuki .
Mke wa ankal Michuzi akisoma risala fupi kwa niaba ya Muhidini Issa Michuzi ambaye ameukubali sana uchakarikaji wa Mwanadada Shamim Mwasha mpaka kufikia hapo alipo mpaka sasa.
Muwakilishi kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd,Harriet Khopa akizungumza machache kuhusiana na kinywaji cha baileys kinachotengenezwa na kampuni hiyo,ambayo pia kupitia kinywaji hicho, kilikuwa ni sehemu ya udhamini wa hafla ya kutimiza miaka 5 ya 8020 Blog.
Mgeni rasmi,Mbunge wa Viti Maalum,Mh Angellah Kairuki akimkabidhi cheti Mbunifu wa mavazi Binti Afrika,kwa mchango mkubwa katika tasnia ya mitindo hapa nchini,ambapo Shamim alipata nafasi ya kuwapa heshima wabunifu mbalimbali waliotoa mchango mkubwa katika fani hiyo.
Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM),Mh Angellah Kairuki akisoma hotuba yake fupi kuhusiana na tukio hilo adhimu la kutimiza miaka 5 kwa mwanablog mwenzetu,Shamim Mwasha a.k.a Shamim Zeze.
Mmiliki wa 8020 Blog,Shamim Mwasha akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee mchana huu.

Wageni waalikwa mbalimbali wakjimwaya mwaya mchana wa leo kwenye hafla fupi ya 8020 Blog ambayo ilikuwa inatimiza miaka 5 tangu kuanzishwa kwake.
Dj Peter Mo akiangusha mangoma ya nguvu ndani ya hafla hiyo mchana huu ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.




Shami Zeze ambaye ndiye mmiliki wa 8020 Blog inayotimiza miaka 5 tangu kuanzishwa kwake akimkabidhi cheti che heshim Mke wa Ankali Michuzi pichani kati huku mgene rasmi akishuhudia,Mh.Angellah Kairuki
wageni waalikwa wakifutuatilia matukio yanayoendelea ukumbini hivi sasa.
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo.
Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM),Mh Angellah Kairuki pichani kulia akiongoza wageni waalikwa katika chakula cha mchana kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 5 ya 8020 Blog,Diamond jijini Dar.
Wageni waalikwa mbalimbali wakipata chakula cha mchana kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 5 ya 8020 Blog inayomilikiwa na Mwanadada machachari na makini katika mambo ya fasheni na urembo,Shamim Mwasha a.k.a Zeze ndani ya ukumbi wa diamond jubilee mchana huu.



©Fredy Njeje